Makahama ya Misri imetoa hukumu kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi kutokana na kuuawa kwa waandamanaji wengi wakati akiwa madarakani.
Hukumu
hiyo iliolewa leo kwa Rais huyo tangu aondoke madarakani mwaka 2013
kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake sasa
amehukumiwa jela miaka 20.
Yeye pamoja na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood
walilaumiwa kwa kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi wa habari na
waandamanaji wa upinzani wakati wa vurugu nje ya ikulu ya nchi hiyo
mwishoni mwa mwaka 2012.
Wakati umati ulipokusanyika nje ya ikulu bwana Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya hivyo.
Kabla ya kutolewa hukumu leo, Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa Abdul Fatta al-Sisi kwa kutumia mahakama kama silaha.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment