Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Shape ya Shilole Yazua Vimaneno Msiba wa Kapteni Komba..Mwenyewe Adai ndivyo Alivyo

Shape ya Shilole Yazua Vimaneno Msiba wa Kapteni Komba..Mwenyewe Adai ndivyo Alivyo

MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amepondwa vibaya katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mhe. Kapt. John Komba, baada ya kuvaa kigauni kilichombana na kumuonyesha maungo yake ya mwili mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Baadhi ya watu waliofika katika Viwanja vya Karimjee vilivyopo Posta jijini Dar, walianza kunong’onezana baada ya mwanamuziki huyo kujitokeza mbele na kuimba kipande cha shairi lake huku wakisema kuhusu kigauni alichovaa bi’dada huyo.

“ Jamani hii aliyovaa si ‘tight’ kabisa, maana yupo tofauti na wenzake ambao wote wamevaa nguo za heshima zinazowasitiri  maumbo yao, kwa nini yeye ameamua kuvaa hivyo?” alisikika mama mmoja ambaye naye alikuwemo kwenye maombolezo.

Paparazi wetu alimtafuta Shilole na kumuuliza kuhusiana na hilo alisema hakuvaa vibaya isipokuwa alionekana vile kutokana na umbo la mwili wake ndio lilivyo..... WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips