Moja ya sababu inayoifanya CCM kuendelea kutawala ni kuwa na hazina ya wapiga kura..huu ni ukweli ulio wazi maana wapiga kura walio wengi ni wakina mama na wakina baba na hawa wengi ni CCM na hata ukichukulia mfano kwenye zoezi ili linalo endelea la uandikishaji wa wapiga kura utagundua kuwa walio hotokeza wengi ni wakina mama na wakina baba ambao wengi ni wapiga kura wa kudumu wa CCM..wapiga kura wa chadema wao wamejaa kwenye mitandao lakini huwa hawaendi kujiandikisha na hawana sifa ya kupiga kura hii huwapa ushindi wa mezani CCM kila leo.
Pili CCM wanajua kutatua migogoro inayo jitokeza bila kuleta madhara ukilinganisha na vyama vya upinzani hasa Chadema na UKAWA..mtu anaweza kujidanganya muda huu kuwa CCM imevurugika oooh CCM kuna makundi na yatakimaliza lakini mkitaka kuhakikisha kuwa CCM itatawala milele na inajua kumaliza makundi subiri muone wakati wakuelekea uchaguzi mkuu ndio hapo kila mtu ataamini kuwa hiki chama kita tawala milele na kama mtakumbuka kipindi kilicho pita kabla ya Jk kulijitokeza makundi mengi lakini yalikwisha na CCM ikasonga mbele wakiwa wamoja...tofauti na UKAWA hasa Chadema hawana uwezo wa kuhimili vishindo vya makundi bila kuleta madhara na mkitaka kuamini subirini wakati wa kumpata wagombea mbalimbali kuputia UKAWA hasa mgombea Urais hapo ndio mtaamini UKAWA hawana uwezo wa kuhimili makundi na watasambaratika au watakwenda wakiwa wamegawanyika kabisa na ndio maana hadi sasa hakuna anaye onesha nia ya kugombea hasa Urais maana wanajuana walivyo(patachimbika)
Tatu CCM wana hazina ya viongozi ambayo ni ndefu kwa hiyo wana uwezo wa kuuwa makundi kwa kuwaacha wote walio kwenye makundi na kuchagua mtu ambaye hatoki kwenye makundi na wakaendelea kutawala milele...maana njia pekee ya kuuwa makundi ni kujichinjilia mbali wote walio kwenye makundi na kuchukua mtu tofauti na wote wata tulia maana kila mmoja kakosa..lakini huko UKAWA safu ni nyembamba saba kiasi kwamba ni vigumu kuchagua nje ya makundi hasimu..mfano UKAWA kuna kundi la Slaa , na Lipumba..ukiwatoa hawa hakuna mwingine mwenye sifa au anaye weza kugombea kiti cha Urais sasa kazi inakuja jinsi ya kuunganisha haya makundi bila kuleta mpasuko ni ngumu maana nje ya hao hakuna na ukipendekweza mmoja kati ya hao bado kutakuwa na mpasuko na hapo ndio mtakubaliana nami kuwa CCM itatawala milele..
Nne CCM ina umoja wa vijana ambao ni hazina,hai na wenye nguvu...hapa pia ndipo CCM inapo tofautiana sana na UKAWA ambao wamejaza vijana wengi lakini ni wapiga kelele tuu na wengi wao kujiandikisha hawaendi na hawana sifa za kupiga kura halafu wengi wao wana nunulika kirahisi..kwa mfano ukiangalia Bavicha ni kama imekufa kabisa tota aondoke Heche imekufa kabisa kazi zote zina fanywa na wazee ..Bavicha wameponzwa na makundi ya kugombea uenyekiti na ndio yanao utafuna umoja huo kiasi kambwa mwenye kiti wao ana kosa ushirikiano na anashindwa kuwaunganisha vijana.. Bavicha wengi wanacho fahamu ni kuongea kama Mbowe tuu ...pia huu ni ushahidi CCM kutawala milele..
Tano CCM wanajua jinsi ya kujipanga na kukabili yanayo wakumba hasa maswala ya ufisadi wa baadhi ya wanachama na huja na suluhu ndio maana hata wakienda kwa wananchi huwa sikiliza lakini tofauti na UKAWA hasa chadema huwa hawana majibu zaidi ya kuadithia story za ufisadi na hawana lingine la kuwambia wananchi zaidi ya story za ufisadi na ni waongeaji sana kuliko vitendo hivyo hilo linawafanya wananchi wawachoke na waonekanae hata wakipewa nchi nao watakula tuu!
Pia kuna sababu tano zitakacho kifanya chama cha ACT kuwa chama kikuu upinzani kuanzia October...
Kwanza ACT kinatangazwa sana na kupewa airtime na vijana wa chadema kiasi kwamba kila mtu anataka kukifahamu na watu wametamani sana kujiunga na hiki chama kipya ambacho kina isumbua chadeema kiasi hiki hadi wana sahau mambo yao..
ACT kitapata majimbo mengi hasa ya upinzani hasa ya chadema kutokana na nguvu aliyo nayo bwana Zitto kabwe na hivyo atawashawishi sana wananchi na watakichagua maana kila mtu anajua nguvu ya Zitto kwa wananchi hata UKAWA wana fahamu hilo.
ACT itakuwa kimbilio la vijana wengi kutokana na nguvu ya Zitto na bila shaka hili halina ubishi kwa kuwa ni wazi kuwa Vijana wengi walio chadema wamepwnda siasa na wameipenda Chadema kupitia Zitto na walivutiwa na Zitto kutokana na uwezo wake mkubwa katika siasa hivyo wengi watajiunga nae na hapo Chadema hawato amini bali wajiandae sana kwa upinzani mkubwa...wabunge wengi vijana wa chadema wamepata ubunge kwa kupitia nguvu ya Zitto na hilo hawawezi kubisha.
Tatu ACT imepata mtu mwenye ushawishi mkubwa na mwenye uwezo wa kujenga hoja kuliko kiongozi yeyote yule wa upinzani..Zitto ni mtu aliye barikiwa nguvu ya ushawishi kabisa kila mtu anajua anapo simama kuongelea jambo kila humvuta kila mtu bila kujali itikadi yake ...tofauti na kule chadema ambapo wote wameigana jaziba hakuna anaye weza kuongea jambo bila jaziba au munkari hili litakifanya chama cha ACT kuwa chama kikuu cha upinzani..
Nne ACT imepata pakujifunza maana wameona wenzao hasa chadema walipo kwama hasa uwezo mdogo wa kushawishi watu kuwapigia kura....maana chadema hawana njia nyingine ya kushawishi watu zaidi ya kusema ufisadi na hii imewachosha watu maana watu wanajua hata wao si wasafi lakini kwa timu ya ACT hakika kutakuwa na suluhu hivyo chadema wata sahaulika.
Mwisho ACT kitajengwa sana na walio kosa haki zao chadema hivyo wataona ni sehemu ya kukimbilia ..pia wabunge wengi au vijana watakao kosa nafasi kutokana na mfumo wa chadema wa kuwapata viongozi au wabunge ambao hautoi haki ACT itakuwa kimbilio lao!WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment