Amesema, Zitto ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Bara na naibu kiongozi wa upinzani bungeni, anafanya kazi asiyoifahamu na ambayo haina mavuno.
“Ninamfahamu vizuri. Wakati tuhuma hizi za usaliti zilipoanza kuibuka, Kamati Kuu ilinikabidhi jukumu la kumsaidia mama yake mzazi kumlea kijana huyu.”
Kauli ya Baregu ilitolewa siku moja baada ya Zitto kujiondoa bungeni na baadaye kujiunga na Chama cha ACT – Tanzania.
Prof. Baregu aliwahi kuwa “mlezi wa Zitto” ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alikabidhiwa jukumu hilo na Shida Salum, mama mzazi wa Zitto (marehemu), baada ya mama huyo kuiomba Kamati Kuu (CC) ya chama hicho “kusaidia kumlea.”WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment