Kwa kauli hiyo, ni sawa na mama watoto hao kuchukuliwa kama bahasha maana bahasha ikishafikisha barua, inakuwa haina umuhimu tena bali kinachofanyiwa kazi ni barua iliyokuwa ndani.
Binafsi kama mwanaume sikufurahishwa na kauli kama hii kwamba hataki mazoea na mwanamke bali mapenzi ni kwa watoto, na je kama si huyo mwanamama hao watoto angeweza kuwazaa mwenyewe.
Huu pia ni ujumbe kwa wale wenye tabia kama za huyu jamaa na pia wale wanaotelekeza mama na watoto wanaenda kutafuta mwanamke mwingine.
Mtoto anahitaji malezi ya wazazi wote labda itokee bahati mbaya mmojawapo kafariki lakini unakuta mtoto anateseka, pimbi anadunda mtaani.
Je wewe unamwunga mkono Ney wa Mitego kwa kauli yake. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment