Baraza
la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Kilimanjaro Premium
Lager wamezindua rasmi msimu mwingine wa tuzo za muziki Tanzania
unaojulikana kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA).
Meneja wa bia ya Kilimanjaro Pamela Kikuli amesema; “Kilimanjaro
Premium Lager ni bia ya watanzania na imejikita katika kuwaletea
burudani na pia kutoa majukwaa ambayo yanawapa Watanzania fursa ya
kukuza vipaji mbalimbali.. hii tumeithibitisha kwa juhudi za makusudi za
kutenga fungu kubwa na kuongeza ushiriki wa wataalaam mbali mbali
kwenye fani husika ili kuziendeleza, kuzikuza na kuziongezea thamani
tuzo hizi mwaka hadi mwaka sambamba na umaarufu kuongezeka kwenye medani
za Kimataifa.”
Kampuni hiyo imewekeza zaidi ya Tshs. Bil.1 kuhakikisha ubora wa hali ya juu unajitokeza kwenye mchakato mzima wa tuzo hizi.
Msimu huu hauna mabadiliko makubwa sana
katika vipengele wala mfumo wa kuwapata wasanii watakaoshiriki, kuna
maboresha kwenye njia za upigaji kura kwa mfano kwa sasa ni watu wengi
wanatumia Whatsapp, KTMA imewarahisishia kwa kuongeza njia hiyo kwenye
mchakato wa kupendekeza na kupiga kura.
Kura za maoni zitaanza kupigwa tarehe
March 30 ambapo shabiki ataweza kupendekeza nani ama nyimbo zipi ziwemo
kwenye vipengele vyote vya KTMA 2015.
Watu watapiga kura kupitia mtandao,
Whatsapp na SMS na utaratibu uliopo ni kwamba namba moja ya simu
itatumika kupiga kura moja kwenye kila kipengele.
Hizi ni njia ambazo utazitumia kupiga kura;
- Whatsapp – 0686 528 813.
- SMS – 15415.
- Mtandao – www.ktma.co.tz
BASATA wamesisitiza usimamizi mzuri wa nyimbo zinazoingizwa; “Kama kuna wimbo ulifungiwa na BASATA hautaruhusiwa kushiriki kwenye mchakato“– BASATA.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment