Shirikisho la soka nchini England FA limekusudia kuweka sheria itakayopunguza idadi ya wachezaji kutoka nje ya nchi za Umoja wa Ulaya watakaosajiliwa katika ligi kuu za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa shirikisho hilo Greg Dyke
amesema kwamba ligi kuu ya England ipo kwenye hatari ya kutowasaidia
wachezaji raia wa Uingereza kama hatua za kupunguza wageni
hazitachukuliwa mapema na sheria hiyo itaanza kutumika May 1 mwaka huu.
Katika mpango huo pia FA itaweka sheria ngumu kwa wachazaji wenye vipaji kutoka nchi nyingine waliokulia nchini humo.
Mikakati hiyo piaimelenga kuimarisha
timu ya taifa ya England ambayo imekuwa haifanyi vizuri kwenye mechi za
kimataifa ikiwemo kombe la dunia.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment