Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Waganga wa Jadi Wawapinga Mkwara Jeshi la Polisi, Wasema Tabia ya Kufanya Msako na Kuchukua Vibuyu vya Itawatokea Puani

Waganga wa Jadi Wawapinga Mkwara Jeshi la Polisi, Wasema Tabia ya Kufanya Msako na Kuchukua Vibuyu vya Itawatokea Puani

Polisi na Vifaa vya waganga wa Jadi
Wakati msako wa kuwakamata waganga wapiga ramli chonganishi ukiendelea nchi nzima hasa katika mikoa ya kanda ziwa, jeshi la polisi nchini limepewa onyo toka kwa wanganga wa jadi juu ya vifaa vinavyokamatwa wakati wa msako wao.

Jeshi hilo limepewa tahadhari ya kukumbana na hatari yeyote baadaye ikiwa wataendelea kukamata vifaa hivyo vikiwamo vibuyu, vitambaa vyeupe na vyeusi, ngao, mikuki pamoja na shanga huku likitakiwa kurejesha mara moja baadhi ya vifaa hivyo ambavyo vimekamatwa.
Katibu mwenezi wa chama cha waganga wa tiba asili nchini, (Chawatiata), Steven Sebastian kutoka Mwanza, akizungumza katika mkutano wa waganga wa jadi wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu, amesema kitendo cha kuchukua vibuyu vyao, kutawafedhehesha.

Sebastiani akizungumza mbele ya kamanda wa polisi mkoani hapa, Charles Mkumbo, amesema kitendo kinachofanywa na jeshi hilo cha kukamata vifaa hivyo, ni kitendo cha hatari kwani kinaweza kusababisha hali ya migogoro mikubwa kati ya jeshi la polisi na jamii.
Sebastian alieleza vibuyu, vitambaa vyeupe, na vyekundu, shanga, ngao, pamoja na mikuki ni vifaa ambavyo waganga hao walirithishwa na wazee wa zamani ambao alieleza vifaa hivyo walivitumia katika kutafuta uhuru.

Akizungumzia hilo, kamanda wa polisi Mkumbo amesema siyo kweli waganga wa jadi wanaonewa ama kusingiziwa wanapiga ramli chonganishi, bali kutokana na uchunguzi wao wamebainika kuwapo na hali hiyo. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips