Samatta ambaye alipata nafasi ya kufanya majaribio katika klabu ya CSKA Moscow ya Urusi mwezi uliopita amepewa ofa nyingi barani ulaya na kama ataendelea kuchezea TP basi atakuwa ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi barani Afrika. Hivi karibuni kuna vyombo vya habari ambavyo viliripoti kuwa mchezaji huyo ana furaha kuendelea kuichezea TP lakini amesema huo ni uzushi mkubwa.
” Sina furaha hapa ( TP Mazembe) nitaondoka wakati wa majira ya usajili katikati ya mwaka na sitaongeza mkataba” anasema Samatta. Ni wapi anakwenda, nini kinachomuondoa TP Mazembe, tafadhaLi endelea kufuatilia mtandao huu wa www.shaffihdauda.co.tz... Utapata kujua wapi mchezaji huyo anakwenda. Je, tayari ameruhusiwa na Katumbi Moies mmliki wa TP?….. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment