Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Showing posts with label Lemutuz. Show all posts
Showing posts with label Lemutuz. Show all posts

LEMUTUZ Aelezea Sababu ya Kutosomeshwa na Baba yake Ambae Alishawahi Kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mzee Malecela

William Malecela, maarufu kama Lemutuz Nation au "King of All Bongo Social Networks" kama anavyofahamika katika mitandao mbalimbali ya kijamii ameeleza sababu za yeye kutosomeshwa na baba yake mzazi.

Le Mutuz Nation ambaye ametumia muda mwingi kusoma na kuishi nchini Marekani na Belgium, ameweka bayana katika kipindi cha Mlimanidotcom cha Mlimani TV kuwa alijisomesha kwa kupitia fedha ambazo zilitokana na kazi mbalimbali ambazo alikuwa akifanya kama vile udereva wa mabasi makubwa huko jijini New York pamoja na kukaanga kuku.

Alipoulizwa kuhusu taarifa za yeye kujisomesha kupitia kuendesha malori na kukaanga kuku, Le Mutuz alisema “Liko sawasawa, unajua ni la ajabu Tanzania lakini si la ajabu nchi nyingine kwasababu mimi wakati nakua, tulikuwa kwenye siasa ya ujamaa kwa hiyo mambo mengi yalikuwa yamebana na mimi nilikuwa nataka ubaharia”

Alieleza kuwa sababu kuu ni kuwa yeye alitaka ubaharia lakini baba yake hakutaka yeye asome masomo hayo katika ngazi ya chuo kikuu, Lakini pia ameeleza kuwa baba yake ambaye ni Waziri mkuu wa zamani wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hakumsomesha kwasababu kipindi yeye anakua ilikuwa ni kipindi cha ujamaa na mambo mengi yalikuwa yamebana hivyo baba yake asingeweza kumlipia kusoma nje ya nchi.

Pamoja na kueleza hayo, Lemutuz alizungumzia sababu za yeye kuliburuza gazeti la Kiu mahakamani na pia kwanini anapenda kupiga picha na wanawake na kuweka Instagram3

Lemutuz Awapa Makavu Laivu Wabongo wa Hapa na wale Waishio Nchi za Nje Wenye CHUKI, WIVU, FITINA, NA HUSDA

Ok I love talking reality kwa mfano niliamua kwenda Ulaya mwenyewe nikapigana mpaka nikaenda mipango yangu ya kwenda kwa kuogopa isiharibike nikaifanya kwa siri sana sikumuambia hata Baba yangu mzazi na siku moja nikaondoka na Sabena Airways enzi hizo mpaka Belgium ndio nikawashitua Washikaji kuwa nipo MBELEZZ hahahha....wiki iliyofuata nikaanza kusikia maneno ya kutisha na kunichafua from my very close friends wakasema na wakaapa sitaweza kuishi Majuu hahaha nikaishia kuishi miaka 30 na Degree 3 juu ya gademu kichwa changu walichokuwa wanakiponda sana....ok one day baada miaka 30 majuu nikaamua kurudi home sweet.home bongo kule majuu sikumuaga mtu walahi washikaji wangu kabisa wabongo kule majuu walipojua nimekirudisha wakaanza matusi mazito na mpaka my ex wife wakaapa kwamba siwezi kuishi bongo nitageuza tu majuu..hahahah guess what nipo hapa Mwaka wa.4 sasa na wanaisoma at Social Media kila.siku habari yangu hahahaj na thanks God nipo vizuri.....now seriously naomba kuuliza Wabongo tuna nini hasa kinachotusumbua mioyoni mwetu mpaka tunakuwa na CHUKI, WIVU, FITINA NA HUSDA hivi I mean hata walioko majuu ungetegemea wamebadilika.lakini wapi WHY TUKO HIVI na TULIFIKAJE HUKO KWENYE ROHO NYEUSI.HIVI? - le Mutuz3

Lemutuz Apinga Matokeo ya Tuzo za Watu Adai Matokeo Yamepangwa..Ali Kiba Hawezi Mshinda Diamond Kwa Kupendwa

Kama mjuavyo hakuna tunzo inayo kosa mikasa na maneno na hii uonesha jinsi tunzo zinavyo wagusa wengi!

Na Tunzo iliyokuwa ina wagusa wengi ni tunzo ya msanii wa kiume anaye pendwa na wengi ambayo imekwenda kwa msanii Alikiba!
Baada ya utoaji wa tunzo huo wengi wamesema na kunena lakini leo hii kuna kitu kipya kimezuka ambacho kinaweza kuwa kivutio kwa wengi na wengi watatamani kujua kilicho nyuma ya haya yote!

Mh Lemutuz au Sauti ya Umeme amesema wazi kabisa kwenye Tunzo za watu haki haikutendeka kabisa na hakuna msanii anayependwa Tanzania zaidi ya Diamond!

LEMUTUZ AMEANDIKA HAYA KUHUSU TUZO HIZO:

Well, thank "Tuzo za Watu" for the best Show but I have a big problem kuamini kwamba1. Millardayo hakupata zawadi zote isipokuwa ya Blogu tu 2. Ali Kiba ameshinda Tuzo ya Mwanamuziki anayependwa against The King Of Pop in East Africa 3. Mzee Majuto kashindwa kupata hata zawadi moja.....nilichokiona ni Manouver and Manipulation by somebody very powerful behind the scene anayetaka ku create a balance katika Field ambayo ni unbalanced by Nature and TALENT in the end ni kuvuruga competititon ambayo tayari ipo na kuwakatisha tamaa waliofanikiwa kwa VIPAJI VYAO...the Idea inatakuwa kuwa ni kupiganisha Vipaji uwanjani sio ku balance the Field from somebody's Office....mapokezi ya Diamond leo Mwanza na LONDON WIKI ILIYOPITA ni EVIDENCE ya kutosha kwamba HAKUTENDEWA HAKI NA TUZO ZA.LEO.....ninawaheshimu sana watayarishaji wa Show ya leo lakini NAOMBA KUKUBALI KUTOKUBALIANA NANYI na we remain kool SIAMINI KWAMBA MATOKEO YA LEO YALIKUWA FAIR na nitashukuru sana kuona process iliyotumika kufikia matokeo ya leo!

...UPDATE: well nimesoma arguments nyingi against my prior post kuna wachache sana wanaojaribu ku make a sense lakini at the end of the heart of all the TRUTH STANDS alone kwamba kulikuwa na unfairness I mean eti KING MAJUTO ana mpinzani Tanzania? Please eti Millardayo ana mpinzani Tanzania? Diamond Platznumz ana mpinzani Tanzania? hahahahahahah that is a joke infact the biggest joke of my life...I mean wananchi wanajaa kwenye Show za Diamond kuliko za Wasanii wote Tanzania lakini hawakumpigia kura? hahahahha ninasema that is.the biggest joke of all the times Diamond ana followers wengi Instagram na FACEBOOK kuliko MTANZANIA YOYOTE ALIYEWAHI KUISHI.HAPA NCHINI lakini hawakumpigia kura? hahahahahha kuna mtu hukoooo anataka niamini that! hahahahah wanannchi wamekubali kununua meza kwa Shillingi Millioni Tatu kumuona Diamond lakini hawakumpigia kura? Ipi ni kazi ngumu kupiga kura kwenye simu au kulipia meza Shillingi Millioni Tatu?......I mean hata aliyetaja washindi alikuwa anatetemeka kutaja kushindwa kwa Diamond WHY? hahahahaha baada ya Category ya Diamond kupita ilikuwa ni rahisi kutabiri the rest of the TUZOS kila mtu alijua mapema kuwa Millard ameshinda blog WHY?....KIPAJI kinatakiwa kushindanishwa na KIPAJI sio otherwise....sina muda wa kujibu low arguments za Yanga na Simba eti mtumzima.na akili zako.unaweza kusimama na kusema Mwanamuziki anayependwa Tanzania sio Diamond eti kuna mwingine! hahahahahahahha namshukuru Mungu kwa kunijalia kwenda Shule niliyoyaona leo ni aibu tupu na ndio mwanzo wa kuua vipaji soon tutaanza tena kuwarudia kina Kandabongo Man ambaye huko kwao huwa.anapiga bure kwenye harusi...sio kosa la Diamond kwamba amewaacha wasanii wenzie maili 20 ni kosa la KIPAJI CHAKE kipaji hakitengenezwi na TUZO ila kukubalika na wnanchi ninasema DIAMOND NDIYE MWANAMUZIKI ANAYEKUBALIKA.KULIKO WOTE TANZANIA NI FACTS NA MIFANO IPO WAZI ni maoni yangu kama huyakubali andika FACTS sio ushabiki wa Yanga na Simba! - le Mutuz3
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips