Badala yake, alitaka Manispaa ya Kinondoni iweke utaratibu wa kuwaongezea walimu fedha za usafiri kwenye mishahara yao ili wajilipie wenyewe.
Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Paul Makonda kutangaza kuwa walimu wa shule za Serikali za Dar es Salaam watasafiri bila kulipa nauli kwenye daladala.
Katika mpango huo ambao umepangwa kuanza Jumatatu ijayo unaozigusa pia manispaa za Temeke na Ilala, walimu watapatiwa vitambulisho maalumu vyenye saini ya Makonda.
Akizungumza katika mahojiano maalumu juzi, Mtulia alisema licha ya kuwa wazo lililenga kuwasaidia walimu, lakini litawasababishia dhihaka.
Alisema kinachopaswa kufanyika ni kutafuta suluhisho la kudumu la kero zinazowakabili walimu ambazo zinachangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.
“Itafika hatua kondakta atamsimamisha mwalimu kwenye kiti kama ilivyo kwa wanafunzi kwa sababu tu halipi nauli… Wazo hili ni zuri lakini lilipaswa kuboreshwa kama kweli nia ni kumsaidia mwalimu,” alisema.
Alisema ikiwa kweli nia ni kuwasaidia walimu, basi halmashauri zina wajibu wa kuhesabu siku za kazi na kiasi ambacho mwalimu atalipia nauli ili fedha hizo ziongezwe kwenye mshahara wake.
Alisema njia hiyo itakuwa ya heshima zaidi kuliko walimu kusafiri bure kwa kutumia vitambulisho kama walivyo wanafunzi wao.
Hata hivyo, alisema ipo haja kwa viongozi wa manispaa hiyo kukaa meza moja na walimu ili kujua changamoto zinazohitaji suluhu ya haraka, akisema huenda nauli ikawa si ya msingi kwao. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment