Dr. Slaa: Nitaendelea kupigia kelele mambo yanayohusu taifa langu
Dr. Slaa: Uchaguzi huu ni wa kipekee. Watanzania wanataka mabadiliko. Umma haujatafsiri maana ya mabadiliko
Dr. Slaa: Dhana ya mabadiliko haijaelewa vyema. Dhana hii si mpya. Ilisemwa hata na Hayati Mwalimu Nyerere
Dr. Slaa: Mabadiliko yana sura mbili. Yapo ya kutoka pazuri kwenda kubaya na ile ya kutoka kubaya kwenda kuzuri. Anatoa mfano wa Dikteta Benito Mussolin wa Italia
Dr. Slaa: Ninahisi tafsiri ya mabadiliko haijaeleweka. Hata wasomi hawaelewi. Kwa upande wa wenzetu wapinzani wanachukua mifano ya hata Marekani ambapo Obama alikuwa na sifa..
Dr. Slaa: Msingi wa mabadiliko ni kutoka ulipo kwenda mahali kwingine. Kwenda kuzuri. Kuna dhana ya mabadiliko na mapinduzi. Kuna kauli za kutishia kuingia barabarani
Dr. Slaa: Wapo wenye tamaa ya kwenda Ikulu. Hiyo si ambition ya uongozi. Ambition inaambatana na maandalizi
Dr. Slaa: Kumchagua Rais si suala dogo. Tutavumilia kwa miaka mitano
Dr. Slaa: Amani inapaswa kuwa ajenda kuu kwakuwa ni zao la demokrasia.
Dr. Slaa: Naungana na Jaji Warioba kuwa rushwa ilikuwa inatisha. Serikali za Mitaa hupewa asilimia 23 za bajeti. Asilimia 75 ya 23 hupotea kwa rushwa. Kuna grand na petty corruption. Rushwa ndogo huumiza kuliko kubwa kwakuwa zinagusa watu wanyonge.
Dr. Slaa: Katika kampeni za mwaka huu,chama changu CHADEMA kimeacha ajenda ya rushwa. Hata nyimbo za hamasa za kupinga rushwa hazisikiki. ACT ni kama wanairithi CHADEMA kwenye ajenda ya rushwa. Nampongeza Zitto na chama chake. Yuko committed
Dr. Slaa: Msingi wa mabadiliko ni kutoka ulipo kwenda mahali kwingine. Kwenda kuzuri. Kuna dhana ya mabadiliko na mapinduzi. Kuna kauli za kutishia kuingia barabarani
Dr. Slaa: Dr. Magufuli anasisitiza kuwa anapiga vita rushwa. Sijaona jambo hilo kwa CHADEMA. Ukiwa mchafu huwezi kukemea. Dr. Magufuli anasema ataanzisha Mahakama Maalum za rushwa na ukimtazama anaaminika. Dr. Magufuli sijawahi kusema ni msafi. Lakini ana nafuu kati ya wagombea nane
Dr. Slaa: Tulimpinga Rais Kikwete mwaka 2010 kuwanyanyua Mramba,Chenge na Lowassa. Magufuli haogopi kupoteza kura kwa kukemea ufisadi na kusema atawafunga wala rushwa. Magufuli ni jasiri
Dr. Slaa: Kuna michakato inafanyika kama kuwaleta na malori na mabasi. Chama changu kilikuwa hakibebi watu. Lakini kilibeba kwenye mkutano wa Jangwani.
Dr. Slaa: Baada ya kusikiliza na kuona mikutano,kwanza tujiulize tunataka Rais wa aina gani. Mwenye vigezo vya kupambana na rushwa, Magufuli anafaa. Rais hawezi kuongea kwa dakika kumi, nani atakuwa Rais? Ni akina Sumaye?
Dr. Slaa: Tanzania ni mama yetu. Tukichezea amani ya Tanzania,sote tutaathirika. Nawaomba NEC wasimamie sheria. Watanzania tusimamie amani yetu.
MSIKILIZE HAPA KWENYE HII VIDEO:
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment