Katika mkutano huo alitangaza rasmi kujivua Ukatibu Mkuu wa Chadema na uanachama pia wa Chama hicho na kueleza kuwa anastaafu kabisa shughuli za siasa na kwa hiyo akaeleza kuwa hana nia ya kujiunga na chama chochote cha siasa.
Hata hivyo katika kikao hicho ambapo alitumia zaidi ya saa 1 kuongea ambapo alikitumia kikao hicho karibu chote kuporomosha mashambulizi mfululizo kwa chama chake cha Chadema na vyama vinavyounda Ukawa na kumshambulia Edward Lowassa kwa nguvu zake zote na kumuita fisadi mkubwa na kukilaumu chama chake kwa kumpokea Lowassa na kupewa fursa ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Chadema kuwa ni sawasawa na kukihamisha choo kutoka chumbani na kukipeleka sebuleni.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment