Nawasalim wote katika bwana
Wapendwa, yupo msichana mmoja, alimaliza chuo mwaka jana, anakaa mtaa wa nyuma yetu, anatufaham sana mm na mke wangu, lakini zaidi ya yote tunaabudu pamoja, yaani kanisa moja, nilipoanza kuabudu hapo, yy tayari alikua mwenyeji Wa kanisa hilo na familia yake kwa muda sasa
Mara baada ya Mimi kujiunga na kanisa hilo, huyo binti ndie alinipokea, nilijiunga peke yangu, wife yeye aliendelea na kanisa lake la zamani, amehamia kwetu recently
Basi, tukawa tumebadilishana namba zetu na binti, tukaulizana na kuongea mambo mengi ya maisha, nilipomtajia ninapofanya kazi akaomba nimtafutie kazi kwenye shirika letu, nikamwambia nitajitahidi, baade akaniletea CV zake nikazipeleka kwa hr wetu na kumuomba anisaidie nafasi ikitokea, akakubali
Baadae binti akaja na laki mbili kutoka kwa wazazi wake, kwamba nimpelekee hr ya chai ili mambo yaweze kwenda HR akazipokea na kuniomba niwe mvumilivu.
Wakati tunaendelea kusubiri, huyu binti alizidisha sana ukaribu, tukawa wakati mwingine tunachat vitu vya ndani sana, Akawa ananiuliza kama najua hiki au kile ktk love making, Nikawa namjibu kwamba sijui, Basi akadai atanifundisha, ndipo nikashangaa atanifundishaje bila kufanya hilo jambo?
Isitoshe wote tumeokoka.
Nikamwambia kwanza hatupaswi hata kujadili mambo hayo, Pia sikuwahi kutembea na mwanamke mwingine zaidi ya mke wangu baada ya kuoa, akasema ndio maana hujui vitu vingi, tutafundishana taratibu
Kwa kweli sielewi kilitokea nini kuja kuzinduka, bahati mbaya tukawa tumeshafahamiana Mara kadhaa hivi, ukichukulia kwamba nilikua na mgogoro flani na wife kwa kipindi kirefu, kwa ujumla tukawa tumeshafahamiana kama Mara 12 hivi tangu mwanzo Wa mwaka huu
Yule HR wetu kila siku ananipiga kalenda tangu mwezi wa 11 mwaka Jana inakimbilia mwaka sasa, binti ikafika pahala akaanza kusema nimemtapeli, tumekua na ugomvi mkubwa, na unaendelea kukua siku hadi siku, juzi kanitumia sms akidai kwamba eti alimsaliti mchumba wake na kunipa tunda mimi ili nichakarike apate hiyo kazi sasa nimemuingiza mkenge,
Cha kusikitisha zaidi, hili suala linakaribia kumfikia wife maana hapo mtaani kuna watu wamenifuata na kuniuliza.Nashangaa sana, maana hata hilo la kula tunda ni yeye ndio alinirubuni.
Kuhusu hela yake, anadai nimrudishie kwamba wazazi wanaulizia, wakati hela yenyewe alidai tumpe hr ya chai, sasa wadau hela ya chai huwa inarudishwa?Na mimi yule HR tunaheshimiana sana, ni bosi wangu, siwezi kumkoromea, wala kumuimba anirudishie hela yeye anadai nafasi ikipatikana atamuingiza, sasa binti anaona kama ni utapeli muda umekua mrefu
Yote tisa, kumi anadai atakuja kwa bosi wangu kueleza jambo hilo ili aniharibie, na atafanya liwezekanalo mke wangu ajue
Wapendwa msaada wenu please
0 comments:
Post a Comment