Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Vitu Nilivyopenda Kwenye Video Mpya ya ALI KIBA iliyotoka Jana na Kuacha Gumzo Mitandaoni..

Vitu Nilivyopenda Kwenye Video Mpya ya ALI KIBA iliyotoka Jana na Kuacha Gumzo Mitandaoni..

Nimependa jinsi furaha ilivyo tawala kwenye video hii. Nimependa jinsi stylist alivyochagua rangi za nguo za wahusika ambazo zimeendana vyema kabisa na rangi za kuvutia zilizowatala kwenye location. Rangi za nyumba, magari ziko on point balaa – kila kitu kinaonekana kiliweka kwa hesabu kali sana hapa. Navutiwa mno na yule dancer wa kike aliyekuwa anaangalia gari lake lililoharibika na Alikiba aliposogea kutaka kumsaidia wakaanza kucheza, connection na chemistry hatari sana hapo inaonekana – kama wanafahamiana kitambo.

Wale dancers wanaocheza mbele ya kiduka chenye spika mbele yake wako on point. Yule demu point 5 aliyevaa kofia kama ya Michael Jackson yuko on point na kapendeza sana – Alikiba pia anaonekana kummudu vyema. Quality nzuri kabisa inayovutia machoni. Picha hazijapikwa wala nini – natural kabisa! Kimsingi hii ni video kali na niamini kuwa itaufanya wimbo huu kuwa mkubwa zaidi Afrika. I love it. Watch it, Enjoy and stop comparing!
Shout Outs kwa @officialalikiba na director @mejialabi ‪#‎TeamTanzania‬

By Fredrick BundalaWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips