Kwa jinsi nilivyompenda mdogo wake sijui ni nini kilichonifanya nisimwambie.
Nahisi ule usemi wa 'subira huvuta heri' ulinipumbaza, ona sasa kaniwahi dada yake na mdgo wake katambua.
Jamani nilimpenda na bado nampenda mdogo wake ila mazoea ya dada yake kwangu yamechukua sura nyingine.
Niliona njia rahisi ya kumpata mdogo wake ni kuzoeana na dada yake, lakini sasa dada yake kanizoea vibaya .
Hadi kufikia kuniomba namba yangu ya simu haikutosha akaamua kunitamkia kabisa eti anataka kuwa nami bila kujua kama mimi nina malengo na mdogo wake.
Nahisi ndoto zangu kupotea, nipo katika wakati mgumu sana sijui nimjibu vipi dada yake na sijui nitampata vipi nimpendae na wote wanakaa nyumba moja.
JAMANI EEH!
NIMETONGOZWA NA DADA YAKE MSICHANA NINAEMPENDA bado sijamjibu chochote nimekata mawasiliano kwa muda ili kutafakari.
Tafadhali anayeweza kunishauri.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment