Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Nimempata Mwanaume Wa Ndoto Zangu, Alinikuta Nikiwa Kwenye Maumivu ya Mapenzi – Linah

Nimempata Mwanaume Wa Ndoto Zangu, Alinikuta Nikiwa Kwenye Maumivu ya Mapenzi – Linah


Linah akiwa na mpenzi wake Williams Bugeme

Akizungumza na Bongo5 leo, Linah amesema mwanaume aliye naye kwa sasa ni mwanaume aliyekuja kumuokoa akiwa katika wakati mgumu wa kimapenzi.

“Kiukweli malengo yetu ni ndoa na wala haitachukua muda mrefu. Mungu akijalia mwakani,” amesema Linah. “Sasa hivi nataka ndoa mambo ya kuzini sitaki. Mimi sidhani kama ndoa ina ugumu wowote. Nataka sasa hivi kuwa wa halali kwa mtu mmoja na baadaye tupate watoto. Kwa jinsi tulivyoongea kazi ni kazi na mapenzi ni mapenzi, kwahiyo nafasi yangu ya kazi itakuwa pale pale. Na ninafikiri huyu ni mtu sahihi kwangu, ninafikiri ni mtu ambaye anaweza akawa mume wangu ndio maana nimekimbilia ndoa,” ameongeza.

“Amekuja kwangu kama mtu anayenipenda, ameona jinsi ninavyoumia kimapenzi. Kwahiyo huyu amekuja kama mtu mwenye nia, ni aina ya mwanaume ambaye nilikuwa namtafuta kwa muda mrefu na hatimaye amefika, sasa hivi nafurahi.”
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips