Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Mwanamuziki JIDE Ala Bata China Huku Nyumba Yake Akipigwa Mnada Bongo

Mwanamuziki JIDE Ala Bata China Huku Nyumba Yake Akipigwa Mnada Bongo

Deogratius Mongela na Chande Abdallah
GOOD time! Ndivyo unavyoweza kusema ambapo wakati habari ya mjini ikiwa ni kuhusiana na nyumba yake kupigwa mnada, staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ yupo bize jijini Hong Kong, China akila bata, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kampuni ya Udalali ya MEM Auctioneers and General Brokers ilipewa jukumu la kupiga mnada nyumba ya mwanamuziki huyo iliyopo Mivumoni, Kinondoni jijini Dar baada ya Jide kushindwa kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya EFC Tanzania Limited.

Wanahabari wetu waliokuwa na kibarua cha kumtafuta Jide ili kujua anazungumziaje kuhusu nyumba hiyo kupigwa mnada, walizunguka kwenye viunga lukuki vya Dar ambavyo mwanamuziki huyo huwa anapatikana lakini jitihada hazikuzaa matunda, achilia mbali simu yake ya mkononi kutopatikana.

Wakati gazeti hili likielekea mitamboni, chanzo kimoja kilipenyeza habari kuwa staa huyo wa Wimbo wa Yahaya yupo nchini China ‘anakula ujana’.“Kwa taarifa yenu Jide hayupo Bongo, ametimka zake China kula raha kama vipi fuatilieni kwa mbinu zenu mtabaini hiki ninachowaeleza,” kilinyetisha chanzo chetu, Jumamosi iliyopita.

Kabla ya kuwadadisi wadau wengine wa karibu wa Jide, Ijumaa Wikienda liliingia kwenye ‘peji’ ya Instagram ya mwanamuziki huyo na kukutana na posti iliyoonesha kuwa yupo Dubai akielekea nchini China kuinjoi maisha.
“Dubai-Hong Kong leo nimetoa ushamba sikujua mpaka ndege ikipaa kuna WiFi (huduma ya intaneti) tembea ujionee,” aliandika Jide.

Alipotafutwa Gardner G. Habash ambaye alikuwa mume wa Jide alisema kwa kifupi kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na nyumba hiyo kupigwa mnada.
GPL WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips