Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » ALI KIBA Akana Vibaya Kuwa Ana Bifu na Diamond..Adai Alistahili Kushinda Tuzo Alizoshinda KILL Awards na Kumbwaga Diamond

ALI KIBA Akana Vibaya Kuwa Ana Bifu na Diamond..Adai Alistahili Kushinda Tuzo Alizoshinda KILL Awards na Kumbwaga Diamond

Msanii kutoka Tanzania Ali Kiba ambaye amejitokeza tena katika ulingo wa muziki baada ya kupumzika kwa miaka mitatu amepuuzilia mbali madai kwamba alipendelewa katika tamasha la tuzo za Kilimanjaro.
Ali kiba ambaye alipata tuzo sita na kumshinda msanii wa kimataifa Diamond Platinum amesema kamwe hakupendelewa na kwamba ni muziki wake unaopendwa na wengi.
Akizungumza katika mahojiano na runinga ya Citizen siku ya ijumaa usiku nchini Kenya,Kiba amesema kuwa anahisi yeye ndio bora na kwamba ilikuwa haki yake kushinda tuzo hizo.
''Nahisi kwamba mimi ndio bora na nilifaa kushinda tuzo hizi.''Mashabiki wangu waliukosa mziki wangu na ndio maana walinipigia kura na ndio maana nilishinda tuzo sita kati ya saba nilizoteuliwa'',alisema.
Na alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond,Kiba alikana madai kwamba wawili hao hawana uhusiano mwema.
''Sina uadui wowote kati yangu na Diamond na haujakuwa''. Naweza kukuhakikishia kuwa mimi na Diamond hatujapigania kuhusu chochote''.
Hatahivyo amesema kuwa inamkera wakati watu wanapomlinganisha na mwimbaji huyo wa Mbagala.
Alisema:Mimi ni mimi na Diamond ni Diamond WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips