Ralph R. Debbas, ni mkurugenzi wa kampuni mpya ya magari W Motors iliyopo Dubai.
Na baada ya ujio wao kwenye ulimwengu wa magari, kampuni hii imeanza
kutengeneza headlines za kipeke duniani, ikiwa ni kampuni ya kwanza ya
kiarabu kutengeneza magari yanayoipiku brand kubwa za magari duniani
kama Ferrari, Lambroghini na Buggati.
Lykan Hypersport
Toleo la kwanza la gari kutoka kwa W Motors ni supercar Lykan Hypersport,
gari lililotokea kuweka headlines kubwa kwenye mitandao ya kijamii kama
Instagram pamoja na internet na headlines zilizopo sasa hivi ni kwamba
gari hili laweza kuja kuwa gari la kifarhari kushinda yote duniani.
Nimekusogezea baadhi ya picha za gari hili hapa chini ila na wewe uweze kujionea.
Lykan Hypersport ni gari la kwanza kutengenezwa na kampuni ya W Motors iliyopo Dubai
Huu ndio muonekano wa gari hili kwa mbele
Muonekano wa gari hili kwa nyuma
Muonekano wa gari kwa ndani
Mwezi wa sita mwaka huu, Lykan Hypersport lilitangazwa kuwa gari la kwanza la kifahari kutumika na polisi wa Abu Dhabi
Gari hilo sasa hivi lipo kwenye ukaguzi kuona kama litafaa kwa shughuli za kipolisi.
W Motors sasa hivi wako mezani na project nyingine ya gari hii itakayoitwa SuperSport Car, yatakayo tengenezwa 25 tu kwa mwaka.
Kampuni
hiyo inadhamiria kutengeneza matoleo ya magari yatakayo shindana kwenye
soko na matoleo ya Ferrari, Lamborghini na Bugatti.
Gari hili likikamilika litauzwa kuanzia dola 250,000 na litakuwa linatengenezwa Dubai tu kwenye kiwanda hicho kipya.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment