Maisha ni magumu sana huko vijijini. Wanawake wengi wanateseka na familia (wengi sana ni wajane). Na mambo mengine chungu zima!
Kwa kweli nchi yetu tunaonekana huko nje kuwa sisi ni masikini sana!
Kwa Mtanzania kutumia shilingi za kitanzania milioni tatu kwa ajili ya starehe ya kula kulewa na kujianika uchi hadharani kwa siku moja ni kufuru dhidi ya Mwenyezi Mungu na watanzania masikini!
Haya ndiyo mambo yanayopelekea watu kuiba mali ya umma!
Watu waseme watakavyo lakini ukweli ni kwamba kwa umasikini huu tulio nao, kutumia hicho kiasi cha pesa kwa anasa ya siku moja tena kwa watu wasio na mchango wowote kwa taifa ni kufuru kubwa na matusi!
By G SamWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment