Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Not So Fast: Collabo ya Diamond na P-Square Bado Haijatoka, Kumbe Wimbo Uliosambaa ni wa Iyanya

Not So Fast: Collabo ya Diamond na P-Square Bado Haijatoka, Kumbe Wimbo Uliosambaa ni wa Iyanya


Kama umedownload au kutumiwa wimbo unaosemekana kuwa ni wa Diamond featuring P-Square na pamoja na kuusikiliza kwa mara kibao ukashindwa kusikia sauti ya Paul au Peter Okoye, basi sikio lako halikudanganyi – hakuna collabo hiyo.



Wimbo huo unaitwa ‘Marry Me’ ni wa Iyanya ambao kipindi muimbaji huyo wa Nigeria amekuja kwenye Fiesta mwaka juzi, alimpa nafasi Diamond kuingiza kitu kwakuwa alisafiri na producer wake, Tekno aliyetembea na vifaa vya muhimu vya studio. Kwenye wimbo huo Diamond hakuimba serious na infact aliimba freestyle tu, kwa mujibu wa maelezo ambayo meneja wa Diamond ameyatoa kwa Bongo5.

Wimbo original upo kwenye album ya Iyanya iitwayo ‘Desire’ (Iyanya vs. Desire) iliyotoka February 6, 2013. Kwahiyo Iyanya alitaka kutengeneza remix ya wimbo huo ambayo hata hivyo haikuweza kujumuishwa kwenye album hiyo.

Blog kadhaa za Bongo zimeupost wimbo huo kama wimbo wa Diamond aliowashirikisha P-Square kitu ambacho si kweli. Hakuna shaka kuwa hiyo ni collabo inayosubiriwa kwa hamu sana.

Source: Bongo5 WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips