Wanasiasa wa upinzani nchini wamepinga kitendo cha
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kutumia
ndege ya Serikali kwenye shughuli za kichama za
kujitambulisha wakisema hatua hiyo ni matumizi mabaya
ya rasilimali za Taifa. Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema walifuata taratibu
zote kuikodi ndege hiyo na kwamba chama chake ni
kikubwa na hakiwezi kushindwa kukodi usafiri huo.
Source: Mwananchi
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment