Andre Ayew
Mshambuliaji
wa Ghana Andre Ayew amejiunga na kilabu ya Swansea kwa uhamisho wa bure
na kuandikisha mtakataba wa miaka minne na kilabu hiyo.
Ayew
mwenye umri wa miaka 25,amekuwa katika kilabu ya Marseille tangu mwaka
2006 lakini mkataba wake na kilabu hiyo ya Ligue 1 ulikamilika mwezi
uliopita.Mchezaji huyo aliyetajwa kuwa mchezaji bora na BBC mwaka huu alifunga mabao 52 katika mechi 181 katika kilabu hiyo na amelichezea taifa lake mara 62.
''Nilihisi kwamba huu ndio wakati mwafaka kwangu'',alisema Ayew. Nilihisi hamu ya kucheza katika ligi ya Uingereza na kutaka kukuwa kama mchezaji na kwamba Swansea ndio suluhu kwangu kwa njia yoyote''.
"Uaminifu na hamu ya klabu hiyo ulinifanya kujihisi kwamba ni kweli wananitaka.Wameonyesha hilo kwa kila njia''.
0 comments:
Post a Comment