Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la kihistoria mjini Carolina Kusini amekamatwa.
Kulingana
na mwanasheria mkuu Lorreta Lynch,awali maafisa walimtaja kijana huyo
wa miaka 21 kuwa Dylann Storm kama mtu waliyekuwa wakimsaka kwa
shambulizi la Charleston.Maafisa wamelitaja shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki.
Bi Lynch amesema idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini njia mwafaka ya kumfungulia mashtaka mshukiwa.
0 comments:
Post a Comment