Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Jerry Muro Afukuzwa Yanga !!! Ukweli Huu Hapa ..Mwenyewe Atoa Tamko Kuhusu Habari Hizo za Kufukuzwa

Jerry Muro Afukuzwa Yanga !!! Ukweli Huu Hapa ..Mwenyewe Atoa Tamko Kuhusu Habari Hizo za Kufukuzwa


Mkuu wa Kitengo cha habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga,Jerry Muro amekanusha kutimuliwa kwenye klabu hiyo kwa utovu wa nidhamu.

Taarifa zilizoandikwa na gazeti la Uhuru zinasema kuwa habari kutoka kwa mmoja wa viongozi wa klabu hiyo,ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa si msemaji alisema kuwa Muro ametimuliwa baada ya kufanya kazi kinyume na maagizo ya uongozi wa klabu hiyo.

Kiongozi huyo alisema kikao cha dharura cha kumfuta kazi kilifanya juzi jioni kabla ya maazimio kupelekwa kwa mwenyekiti wa klabu hiyo.Yusuf Manji.

Baada ya taarifa hizo Jerry Muro alijibu tuhuma kwa kusema hivi… Ndugu zangu nimepigiwa Simu nyingi Sana na asubuhi hii nimeona Kwenye gazeti ka uhuru kuhusiana na taarifa zangu za kuondoka Yanga wakati natafakari hatua za kuchukua dhidi Ya upotoshaji huu wa Habari naomba niseme Jambo moja Muhimu mimi Bado Niko Yanga Kama Mkuu wa idara Ya Habari na Mawasiliano na mimi Bado mwanachama hai wa Yanga Mwenye kadi No 028508 Niko Yanga na nitaendelea kuwa Yanga Miaka mia,wasalamu jerry muro…. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips