Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Hali si shwari ndani ya FIFA, kashfa zazidi kufichuliwa !!

Hali si shwari ndani ya FIFA, kashfa zazidi kufichuliwa !!

Wapelelezi wanaofatilia kashfa ya rushwa inayohusu shirikisho la soka ulimwenguni FIFA wameahidi kufichua makubwa zaidi baada ya kugundua siri nzito zilizojificha kwenye mchakato wa kuchagua mwenyeji wa kombe la dunia.

Wapepelezi hao wakiongozwa na Mwanasheria mkuu wa Uswisi, Michael Lauber wamesema kuwa kuna matukio karibu 53 ya uchakachuzi na utakatishaji haramu wa fedha ambayo yamegundulika kwenye michakato tofauti ya kumpata mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia na matukio haya yamehusishaa watu wazito ambao kama yatagundulika undani wake yatazua hofu na utata mkubwa.

Mwanasheria huyo ameonya kuwa hatajali kama upelelezi wake utasababisha hasara ya fedha  au kupokonywa uwenyeji kwa nchi za Urusi na Qatar na anachojali ni ufanisi wa kazi yake na si kitu kingine.

Imedaiwa kuwa upelelezi huu unahusisha kuhojiwa kwa viongozi wa juu wa FIFA akiwemo rais wa zamani Sepp Blatter ambaye hivi karibuni alitangaza kujiuzulu siku chache baada ya kuchaguliwa kwa kipindi cha tano.

Rais wa Fifa wakati akitangaza mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 .
Rais wa FIFA wakati akitangaza mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 .

Viongozi kadhaa wa zamani wa FIFA wakiwemo Mmarekani, Chuck Blazer na rais wa zamani wa chama cha soka cha Trinidad and Tobago, Jack Warner wameahidi kutoa ushirikiano kwa wapelelezi huku wakiahidi kuwa watazungumza bila kuficha. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips