Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » FIFA yampiga marufuku Kiungo wa Nigeria

FIFA yampiga marufuku Kiungo wa Nigeria

Ugo Njoku apigwa marufuku ya mechi tatu
Mchezaji wa timu ya wanawake ya Nigeria Ugo Njoku amepigwa marufuku ya mechi tatu.
Kamati ya nidhamu ya FIFA ilifanya kikao chake nchini Canada na kufikia uamuzi huo baada ya kutizama video inayomuonesha Njoku akimpiga kumbo mchezaji wa Australia Sam Kerr katika mechi ya makundi ya kombe la dunia la wanawake .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa mchezaji wa akiba na aliingia uwanjani katika dakika ya 52 ya mechi hiyo ya kombe la dunia.
Japo tukio hilo halikuonekana na muamuzi wa mechi hiyo, kamati hiyo ya nidhamu ilikaa kandokando ya kombe la dunia na kufikia uamuzi huo.
Mchezaji huyo amepigwa faini ya dola elfu tatu na mia mbili $3,200.

  Gallos Official Blog
Chanzo BBC
Mshambulizi wa Ufaransa Camille Abily aliyempiga kumbo mlinzi wa England Laura Bassett hakuadhibiwa.
The Super Falcons ya Nigeria iliambulia kichapo cha mabao 2-0 katika mechi hiyo.
Njoku sasa hataruhusiwa kushiriki mechi dhidi ya Marekani.
Haijulikani kwanini hatua sawa na hiyo haikuchukuliwa dhidi ya mshambulizi wa Ufaransa Camille Abily aliyempiga kumbo mlinzi wa England Laura Bassett.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips