Ilianza kama utani lakini siku zilivyosonga ndivyo
uhusiano wao ulivyowekwa wazi, hao ni watu wawili waliowahi kuwa maadui
wakubwa miaka kadhaa nyuma.
Hapo nawazungumzia staa wa filamu Shamsa Ford na msanii wa
Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ambao kwa sasa wamezama
kwenye mahaba niue.
Awali, wahusika wote walitumia nguvu kubwa kukanusha juu ya
uhusiano wao lakini inatajwa kuwa mahaba yao ndiyo gumzo kuliko ya
wengine wote katika Bongo Muvi na yanashika nafasi ya pili katika Bongo
Fleva nyuma ya Diamond na Zari kwa sasa.
Awali, uadui wao ulitokana na Nay kuwaponda wasanii wa kike
wa Bongo Muvi na kudai wengi wao hawana lolote na kazi yao ni kujiuza,
Shamsa alikuwa mmoja wa waliopokea kwa hasira kali na kumbwatukia Nay
lakini ule usemi kuwa ‘wagombano ndiyo wapatanao’, ulikuwa unawahusu.
Walipoulizwa juu ya mahabati yao baada ya picha kuvunja
mitandaoni wakipeana ‘mabusu’ motomoto hivi karibuni, walisema wana
‘project’ maalum ya filamu.
Sasa inavyoonekana filamu yao imekuwa ya ukweli badala ya zile za kuigiz
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Sasa inavyoonekana filamu yao imekuwa ya ukweli badala ya zile za kuigiz
0 comments:
Post a Comment