Kwa
mara nyingine, Jina la nchi limeendelea kuchafuka baada ya Meli ya MV
Hamal iliyosajiliwa Tanzania kukamatwa barani Ulaya ikiwa imebeba
shehena ya dawa za kulevya aina ya cocaine yenye uzito wa tani tatu.
Kama
dawa hizo haramu zingeuzwa mitaani nchini Uingereza, zingekuwa na
thamani ya Sh1.5 trilioni, kiasi ambacho nchi wafadhili zinatarajiwa
kuichangia Tanzania kwenye bajeti ya mwaka 2015/16.
Matukio
mengine yaliyoichafua nchi ni la meli ya mizigo ya Gold Star
iliyosajiliwa Tanzania ambayo ilikamatwa Septemba 2013, jirani na Kisiwa
cha Sicilia katika Bahari ya Mediterranian nchini Italia wakati
ikielekea Uturuki ikiwa na tani 30 za dawa za kulevya aina ya bangi
zenye thamani ya Pauni 50 milioni za Uingereza (sawa na Sh125 bilioni).
Tukio jingine ni lile la Watanzania wawili kukamatwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6 bilioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, Afrika Kusini.
Tukio jingine ni lile la Watanzania wawili kukamatwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6 bilioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo, Afrika Kusini.
Kiwango hicho cha dawa zilizokamatwa kimeweka rekodi ya ukubwa wa mzigo wa dawa hizo haramu nchini Uingereza.
Awali shehena ya cocaine iliyokuwa kubwa ilikamatwa Septemba mwaka jana ikiwa na mzigo wenye thamani ya Sh450 bilioni.
Awali shehena ya cocaine iliyokuwa kubwa ilikamatwa Septemba mwaka jana ikiwa na mzigo wenye thamani ya Sh450 bilioni.
Kwa
mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, meli ya MV Hamal ilikamatwa
kwenye Bahari ya Kaskazini na baada ya kupekuliwa kwenye bandari ya
Arberdeen nchini Scotland, ilikutwa na shehena ya dawa za kulevya aina
ya cocaine.
Meli
hiyo yenye urefu wa mita 32 na uwezo wa kubeba tani 422, ilikamatwa na
askari wa kikosi cha majini cha Royal Navy waliokuwa kwenye meli ya HMS
Somerset pamoja na askari wa uhamiaji wa Border Force waliokuwa kwenye
meli ya Valiant, karibu kilomita 160 mashariki mwa mji wa Aberdeen
Alhamisi baada ya kupewa taarifa na kitengo cha makosa ya jinai, NCA.
Baadaye,
meli hiyo ilipelekwa bandari ya Aberdeen, ambako maofisa wa Border
Force wenye stadi maalumu ya upekuzi, waliipekua meli hiyo kwa
kusaidiana na polisi wa Scotland.
John McGowan – afisa mwandamizi wa uchunguzi wa NCA, alisema:“Upekuzi
wa meli ulikuwa mrefu na unaosababisha maumivu, na uliofanywa na watu
wenye utalaamu mkubwa wa kufanya kazi kwenye mazingira magumu.
“Matokeo
yake ni ugunduzi huu mkubwa – unaoaminika kuwa mkubwa kuwahi kutokea
kwenye rekodi nchini Uingereza na ambao unaweza kuwa na thamani ya
mamilioni ya fedha.”
Hata
hivyo, rekodi za mtandao wa shughuli za baharini unaonyesha kuwa
katikati ya Februari, meli hiyo ilikuwa Uturuki na wiki mbili zilizopita
ilianza safari kutoka visiwa vya Tenerife nchini Hispania na
ilipokamatwa ilikuwa inaelekea Hamburg, mji wa pili kwa ukubwa nchini
Ujerumani ikitazamiwa kufika jana usiku.
Meli
hiyo imekutwa na watu tisa wenye umri kati ya miaka 26 na 63 wote raia
wa Uturuki na wameshitakiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya.
Washitakiwa wote hawakusema lolote waliposomewa mashtaka yao. Washitakiwa hao ni Mustafa Ceviz, 54, Ibrahim Dag, 47, Mumin Sahin, 45, Muhammet Seckin, 26, Umit Colakel, 38, Kayacan Dalgakiran, 63 na Emin Ozmen, 50, wote wanatoka jiji la Istanbul. Wengine ni Abdulkadir Cirik, 31, anayetoka Mersin na Mustafa Guven, 47, kutoka Yozgat, nchini Uturuki. Walifikishwa mahakamani Jumatatu.
Washitakiwa wote hawakusema lolote waliposomewa mashtaka yao. Washitakiwa hao ni Mustafa Ceviz, 54, Ibrahim Dag, 47, Mumin Sahin, 45, Muhammet Seckin, 26, Umit Colakel, 38, Kayacan Dalgakiran, 63 na Emin Ozmen, 50, wote wanatoka jiji la Istanbul. Wengine ni Abdulkadir Cirik, 31, anayetoka Mersin na Mustafa Guven, 47, kutoka Yozgat, nchini Uturuki. Walifikishwa mahakamani Jumatatu.
Balozi wa Tanzania azungumza
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Akizungumza
na gazeti la Mwananchi, balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Peter
Kallaghe alisema nao wamezisoma taarifa hizo kwenye vyombo vya habari,
lakini licha ya kutokuwa taarifa rasmi kwao waliifanyia kazi kwa
kuwasiliana na mamlaka husika nchini.
Alisema
ni kweli meli hiyo ina usajili wa Tanzania, lakini taarifa walizozipata
toka mamlaka husika zinaonyesha mkataba wa usajili wa meli hiyo
ulimalizika mwaka jana, lakini wamiliki wa meli ama kwa ujanja au kwa
sababu wanazozijua waliendelea kutumia usajili huo.
Balozi
Kallaghe alisema pamoja na kwamba suala hilo tayari liko mahakamani,
wao wanaendelea na uchunguzi kuweza kubaini ukweli kuhusu meli hiyo
kuendelea kutumia usajili wa Tanzania.
Nzowa anena
Mkuu
wa Kitengo cha Kupambana na Kuzuia Dawa za kulevya , Kamanda Godfrey
Nzowa alikiri kuwapo na tukio hilo na usajili wa meli hiyo kuwa
Tanzania, lakini alisema hakuna Mtanzania yoyote aliyekamatwa zaidi ya
Waturuki tisa.
Aliongeza
kuwa, wao kama kitengo cha kupambana na kuzuia dawa hizo wameshaanza
taratibu za uchunguzi wakishikiana na Shirika la Polisi la Kimataifa
(intepol) ili kubaini ukweli wa tukio hilo ambalo halijawahi kutokea
nchini humo.
Hili
ni tukio la pili kubwa la Tanzania kuchafuliwa kimataifa kwa meli
kukamatwa na dawa za kulevya ambapo Septemba 2013 meli ya mizigo ya Gold
Star iliyosajiliwa nchini ilikamatwa ikiwa na tani 30 za dawa za
kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50 milioni
(Sh125 bilioni).
Meli
hiyo ya mizigo ilikamatwa jirani na Kisiwa cha Sicilia katika Bahari ya
Mediterranian nchini Italia wakati ikielekea Uturuki. Maofisa wa polisi
nchini humo walidai kuwa watuhumiwa tisa waliokamatwa ni raia wa Misri
na Syria.
Tukio
hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili kukamatwa na
dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6 bilioni kwenye
Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini.
Siku
za karibuni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kwenye hotuba yake ya
kuahirisha Mkutano wa 12 wa Bunge kuwa kumekuwa na changamoto ya
uharakishaji wa mashauri ya dawa za kulevya, hali inayoifanya Serikali
kufikia hatua ya kufikiria kuwa na mahakama maalumu.
“Nina
imani tukijipanga vizuri inawezekana. Iko hoja kwamba, labda tutafika
mahala tufikirie kuwepo na mahakama maalumu ya dawa za kulevya ambayo
itakuwa na kazi moja tu ya kusimamia mashauri yanayohusu dawa za
kulevya,” alisema.
Waziri
Pinda alisema kati ya mwaka 2010 hadi Julai, 2013, mashauri 368
yanayohusu dawa za kulevya yalipelekwa mahakamani, kati ya hayo, 91
yalimalizika kwa watuhumiwa kufungwa na wengine kutozwa faini.
0 comments:
Post a Comment