Wote watatu tukapelekwa boarding skuli Nairobi-Kenya, mama akarejea nakuru miaka minne baadae mama akakamatwa akarejeshwa arusha kuunganishwa kwenye kesi, mimi ndiye nlikuwa mtoto wa kwanza na woote hatukuwa tumejua kama mama kakamatwa mpaka tuliporudi nyumbani likizo.
Majirani walitushangaa na kuanza kutuuliza alipo mama, kwa msaada tukavunja mlango gari ilikuwepo kuna chumba ilikuwa inafungiwa nliwaambia wadogo zangu mama kaenda kumsalimu mjomba atarejea. Nikaanza misele Nakuru mjini na kiboyfriend changu, siku mmoja akaja mama fulani nlipokuwa nimepaki kigari mjini akajitambulisha ni Mtanzania mmarangu na aliongea kichagga nikazuga simsikii.
Akaniambia amenitambua kwa kuwa anaifahamu gari ya mama na anajua mama na nimefanana na mama.Akanieleza kuhusu mjomba,baba na akaniambia mama alikuwa gerezani arusha kwa kesi. Akanitaka niiuze gari na nyumba fasta kabla havijakamatwa. Akaniambia nsiwe narudi rudi kukaa muda mrefu pale nyumbani mpaka atakapoachiwa mama nlikuwa form three-Nairobi, four days baadae niliuza gari, nyumba ikagoma kwa kuwa collateral ya mkopo alichukua mama benki. Nikawaamuru Madogo tuondoke tuwahi kurudi shuleni mama anatusubiri Nairobi.
With time hata mwaka haukuisha hela ikakata nikashawishiwa na a classmate Elizabeth-Mkenya mkamba wa Nairobi
tukaanza kujiuza likizo and life ikasonga na nikawa nawalipia wadogo na mimi ada. Nilijiuza mpaka nikasoma chuo na wadogo wakaingia sekondari thank god mama aliachiwa baada ya mitatu miaka kuna wakati tuligombana sana na wadogo zangu wakiamini mama amenipa access ya akaunti zake za benki na natumia hela nyingi kivyangu huku nikiwapa wao kidogo.
Tatizo: Kwa sasa tupo Arusha nina boyfriend mmasai na kila wakati wa semina kanisani mchungaji husema ni bora wapenzi wachumba muwekane wazi kuhusu maisha yenu hata ya nyuma ili isiwagharimu baadae. Naogopa sana kumwambia jamaa kuwa niliwahi kuwa nilikuwa changudoa.
NOTE:KUNA WADADA WAKENYA AMBAO NLIJIUZA NAO WAMEHAMIA ARUSHA NA HAWANA KAZI ZA MAANA, nlilazimika kuhama kanisa ambalo mimi nlikuwa kiongozi wa vijana baada ya baadhi yao kuanza kusali pale kanisani uamuzi ambao BF na mchungaji wanaushangaa mpaka leo.Kwa sasa nasali kikanisa kidogo njee ya mji kwa kuwaogopa washirika uchangudoa wenzangu wa NAIROBI...nateseka sana kuwazaWEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment