Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Huddah asema kamwe hawezi kumpost boyfriend wake Instagram kuhofia wajanja wasije kumpora

Huddah asema kamwe hawezi kumpost boyfriend wake Instagram kuhofia wajanja wasije kumpora

Huddah The boss chick amesema kuwa kamwe hatakuja kumuanika mpenzi wake kwenye mtandao wa kushare picha wa Instagram, kwa kuhofia kinadada wajanja wasije kumrubuni na kumnkurunziza kumpindua.

Mrembo huyo kutoka Kenya licha ya kuwa amewahi kushare picha za mwili wake ukiwa mtupu kabisa, amesema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo hawezi kushare na followers wake zaidi ya laki 2, ni mpenzi wake, nyumbani kwake, kitanda chake pamoja na ndugu zake kwasababu huo ni upande wa maisha yake binafsi.

“Never! That is my private. Nyumba yangu, boyfriend wangu, mahali naweka kichwa nalala, utaona tu hotel niko vacation and all that, lakini mahali naweka kichwa changu nalala, na mtu aliyeuteka moyo wangu ni vitu ambavyo kamwe siwezi kuweka Instagram, hata familia yangu siwezi kuwaweka Instagram.” Alisema Huddah kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.


Ameongeza kuwa picha nyingi ambazo huwa anaweka huwa ni za hotelini pamoja na zake mwenyewe, na haweki picha za mpenzi wake kuhofia wasichana wa mjini wasije kumrubuni na kumpora.

Huwa naweka zangu tu, watu wanaona mimi mbinafsi kwasababu huwa siweka picha za watu wengine, kwasababu Instagram ina watu wengine wana matusi sana, wakati mwingine unaweza kuweka picha na rafiki yako wanamtusi rafiki yako, sasa imagine uweke mtu kama boyfriend wako halafu tena wasichana wana competition, wakiona ooh huyu ndio boyfriend wa Huddah, wanataka kumfatilia yule jamaa wanam Dm Dm huko ndani picha uchi zingine halafu bado wanakuja kunitusi, I don’t put my private life out there”. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips