Juhudi
za Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuuvuruga mkutano wa ACT
-Wazalendo jana ziligonga mwamba baada ya Maelfu ya wananchi
kufurika katika viwanja vya Furahisha kuwasikiliza viongozi wa
chama hicho huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika kila kona ya
uwanja huo.
Mpekuzi
ilishuhudia Difenda tatu za polisi zikifanya doria katika
uwanja huo huku polisi wakiwa tayari kwa lolote.
Ulinzi uliimarishwa katika viwanja hivyo kutokana na kauli ya Naibu
Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, John Mnyika aliyoitoa juzi katika
viwanja hivyo ikiwa ni siku moja tu kabla ya mkutano wa
ACT-Wazalendo kufanyika.
Akihutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza juzi ambao
ulihudhuriwa na wafuasi wachache wa chama hicho, Mnyika alisema
Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao’.
Katika hotuba yake, huku akinukuu baadhi ya vifungu vya biblia na Quruan, Mnyika aliwataka wafuasi na wapenzi wa CHADEMA kumkabili Zitto Kabwe kwa namna yoyote kwa kuwa ni adui wa chama chao na ujio wake jijini Mwanza ulikuwa na lengo la kukiharibu chama chao..
Katika hotuba yake, huku akinukuu baadhi ya vifungu vya biblia na Quruan, Mnyika aliwataka wafuasi na wapenzi wa CHADEMA kumkabili Zitto Kabwe kwa namna yoyote kwa kuwa ni adui wa chama chao na ujio wake jijini Mwanza ulikuwa na lengo la kukiharibu chama chao..
“Mtume
Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili na
sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono
Ukawa halafu mnawakaribisha?
“Nendeni kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto.
Sikilizeni niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana
kuanzia EPA mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni
aliyasema haya kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki
Ukawa,” alisema Mnyika.
Zitto Kabwe Ajibu Mapigo
Akihutubia mamia ya wananchi wa Mwanza jana, Zitto alisema kadri siku zinavyosonga wabaya wake wamekuwa wakijionyesha.
Zitto
alisema pamoja na hali hiyo, ACT-Wazalendo haiko tayari kuzungumzia
siasa za wakati uliopita kwa vile kufanya hivyo si afya njema kwa siasa
za upinzani.
Alisema ni vema viongozi wa vyama vya upinzani waachane na ugomvi binafsi na watangulize masilahi ya taifa mbele.
“Mwanzo
walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo likafanyika,
tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili ya kugawa
upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa ajili ya
kuiondoa CCM…wenzetu pia hili hawalitaki sasa ni wajibu wenu kutambua
watu gani hawataki kuiondoa CCM,” alisema Zitto.
Alisema wao (ACT) wana nia ya dhati lakini wenzao wanaweka ugomvi binafsi mbele ya masilahi ya taifa.
“Sisi
ACT Wazalendo bado tupo tayari kushirikiana kwa mujibu wa misingi.
Shabaha yetu ni moja tu, kubomoa mfumo wa uchumi wa kinyonyaji na
ufisadi ili kujenga uchumi shirikishi wa wananchi,” alisema na kuongeza:
“Sikufundishwa
kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani, kufanya hivi
hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana…mmoja kwa kukosa busara
na kwa kuwa aliachana na yule mke anaamua kwenda vijiweni na kutoa siri
za mzazi mwenzie, hili kwetu hapana.
“Tunakuja
na jahazi jipya ambalo ndugu zangu wa Mwanza nimekuja kuwakabidhi,
kubwa tunataka kulirudisha taifa katika misingi yake ya ujamaa na
kujitegemea, tunahitaji ujamaa wa demokrasia,” alisema Zitto.
Alisema
tafsiri ya ujamaa haina maana kuwa chama hicho kitataifisha mali za
watu, bali kitarekebisha makosa ya ubinafsishaji kwa kurejesha mali zote
za taifa zilizouzwa na wanunuzi hawajatekeleza mikataba yao.
Apata Mapokezi ya Kutisha:
Zitto
ambaye amefuatana na Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira,
waliwasili Mwanza saa 8.00 mchana na kupata mapokezi makubwa yaliyoanzia
wilayani Misungwi.
Alipofika katikati ya jiji la Mwanza, Maelfu ya wananchi waliuzia msafara huo na kuanza kulisukuma Gari la Zitto.
Hali hiyo ilisababisha foleni kubwa ambapo trafiki waliingilia kati na kumtaka Zitto Awashe gari kunusuru Foleni.
Alipofika katikati ya jiji la Mwanza, Maelfu ya wananchi waliuzia msafara huo na kuanza kulisukuma Gari la Zitto.
Hali hiyo ilisababisha foleni kubwa ambapo trafiki waliingilia kati na kumtaka Zitto Awashe gari kunusuru Foleni.
Safari
ya kulekea Viwanja vya Furahisha iliendelea ambapo mapokezi hayo
yakiongozwa na vijana waendesha pikipiki (bodaboda) na kikundi cha
wanawake yaliusindikiza msafaa huo hadi ulipoingia kwenye uwanja wa
Furahisha.
Leo ni zamu ya Musoma:
ACT- Wazalendo leo wanatarajia kufanya mkutano wa hadhara Musoma.
Habari tulizozipata zinadai kuwa baada ya CHADEMA Kuvuruga jijini Mwanza juzi, jana walikuwa Musoma ambapo kauli yao ilikuwa ni ileile ya kuwataka wananchi kutohudhiria mikutano ya Zitto Kabwe.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
ACT- Wazalendo leo wanatarajia kufanya mkutano wa hadhara Musoma.
Habari tulizozipata zinadai kuwa baada ya CHADEMA Kuvuruga jijini Mwanza juzi, jana walikuwa Musoma ambapo kauli yao ilikuwa ni ileile ya kuwataka wananchi kutohudhiria mikutano ya Zitto Kabwe.
0 comments:
Post a Comment