Ndani ya wiki moja nimekutana na watu watatu wakitafuta sh.500/= ya 
sarafu kwa sh.2500/= kwa sarafu moja ya mia 5, mwanzoni nilipuuzia 
lakini baada ya kutulia na kufanya utafiti nimegundua kwanza hii sarafu 
imekuwa adimu na inatafutwa kwa udi na uvumba 
Pili ni kwamba wale wapenzi wa SILVER sasa unaweza kupata cheni halisi 
ya silver kwa bei poa kabisa ! sababu ni kwamba zile sarafu za mia tano 
ndio zinayeyushwa na kutengeneza vidani siku hizi
Hii ni KASHFA nyingine kubwa kuhusiana na pesa yetu na mamlaka 
zinazohusika ziko kimya kuhusu hili lakini hii ndio hali halisi 
inayoendelea mitaani TUGUTUKE
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment