Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Kesi ya matumizi mabaya ya mitandao.. mwingine kafikishwa Mahakamani Kenya, katishia ishu ya ugaidi..

Kesi ya matumizi mabaya ya mitandao.. mwingine kafikishwa Mahakamani Kenya, katishia ishu ya ugaidi..

A woman uses an iPad with a Facebook app in this photo illustration in Sofia
Cha mwisho kusikika kutoka kwenye HEADLINES za Bungeni March 2015 ilikuwa ishu ya mjadala wa Muswada wa Matumizi ya Mtandao, mvutano ukawa mkubwa na kusababisha Bunge kuahirishwa saa tano usiku… Wabunge walikuwa wakivutana kuhusu kupitisha baadhi ya vipengele kwenye Muswada huo.
Okay, n’na stori ya Kenya sasa hivi, ishu ni hiyo hiyo kesi ya matumizi ya mitandao.. Kijana mmoja Robert Mungai yeye tayari yuko mikononi mwa Mahakama, kinachosubiriwa ni Mahakama kuendelea kusikiliza kesi yake na kuamua hukumu pia kutokana na jamaa huyo kukabiliwa na kesi ya kuandika ujumbe wa uongo kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya April 4 2015.
Polisi Kenya wamesema Robert aliandika ujumbe wa kuwaonya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Egerton University kilichoko Njoro, ambapo ujumbe alioandika alikuwa akiwataarifu wenzake kuwa Kikundi cha Al-Shabaab kitashambulia.
k fb robert
Robert Mungai
Robert alikataa kutenda kosa hilo lakini Polisi walikataa asiachiliwe kwa dhamana kwa kuwa uchunguzi bado haujakamilika.
Imeripotiwa na vyombo vya habari Kenya, wanasema kwa Sheria ya nchi hiyo ilivyo huenda hukumu yake ikawa kifungo cha zaidi ya miaka ishirini.
Alan Wadi Okengo aliwahi kuingia kwenye HEADLINES pia toka Kenya January 2015 baada ya kuhukumiwa mwaka mmoja jela na kulipa faini kwa kosa la kumtukana Rais Kenyatta mtandaoni.
Ilisikika kwenye show ya TV ya K24 waliripoti hii pia, unaweza kuisikiliza na kuangalia video yake hapa… 




WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Pages (38)1234 »
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips