Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Kauli ya Shibuda kuhusu kuhamia chama Kipya Cha ACT-Tanzania

Kauli ya Shibuda kuhusu kuhamia chama Kipya Cha ACT-Tanzania

Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA), John Shibuda amekataa kuhusishwa na Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), akisema hana mpango wa kujiunga nacho.

Shibuda ambaye ameshatangaza kutogombea ubunge kupitia CHAsdemA katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, amesema “Pamoja na kusema sitagombea kupitia CHADEMA lakini nisilishwe maneno…siendi kwenye chama hicho cha ACT.”

Kauli ya Shibuda imeondoa uvumi ulioenea kwamba angejiunga na ACT baada ya kuwa kwenye mgogoro kwa muda mrefu na CHADEMA.

Akichangia hoja ya muswada wa sheria ya makosa ya mtandao bungeni wiki iliyopita, Shibuda alitumia dakika mbili kuweka sawa uvumi huo akisema, “sitaki kusemewa…nitasema mwenyewe kuhusu mstakabali wangu kisiasa. Huu ni uzandiki.”

Hii si mara ya kwanza kwa Shibuda kuhusishwa na mpango wa kuhamia katika vyama vingine vya upinzani. Mwishoni mwa mwaka jana pia kulikuwa na uvumi kwamba yuko kwenye mazungumzo ya kukinunua Chama cha TADEA kinachoongozwa na Lifa Chipaka.

Hata hivyo, Shibuda alikanusha uvumi huo akisema analishwa maneno. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips