Hasheem Thabeet jina
la kwanza la Mtanzania kuingia kwenye Headlines Duniani akitajwa kama
Mbongo wa kwanza kuchezea Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani, NBA.
Sim Bhullar
unaambiwa ni jina jingine kubwa TENA kuingia kwenye NBA.. Jamaa hatokei
BONGO, ni raia wa Canada ambaye tayari kasaini contract ya siku 10 na
timu ya Sacramento Kings.. wazazi wake wana asili ya India, baadae walihamia Canada ambapo Bhullar alizaliwa mwaka 1992, hivyo anakuwa mchezaji wa kwanza ambaye ana asili ya India kuchezea Ligi ya NBA.
Bhullar ana urefu wa futi 7.5, anakuwa mchezaji wa kwanza kwa urefu kwa sasa hivi, anampita Hasheem Thabeet ambaye ana futi 7.3.
Manute Bol, aliyenyoosha mikono katikati.
Hasheem na Bhullar ni warefu, lakini rekodi ya mchezaji mrefu zaidi aliyewahi kuchezea NBA ni Manute Bol, alikuwa raia wa Sudan alikuwa na urefu wa futi 7.7, alifariki kwa ugonjwa wa ini mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment