Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Hii ndio rekodi iliyovunjwa na mtoto wa miaka miwili India… (Pichaz &Video)

Hii ndio rekodi iliyovunjwa na mtoto wa miaka miwili India… (Pichaz &Video)

dolly-archer_650x400_81427214935 
Mara nyingi wazazi hushauriwa kuona umuhimu wa kukuza vipaji vya watoto wao tangu wakiwa wadogo, taarifa ikufikie kuwa mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameweka rekodi nchini India kutokana na uwezo wake wa kulenga shabaha ya mishale.
_81884282_81884281 
Kutokana na vitabu vya kumbukumbu vya rekodi za taifa hilo, mtoto huyo Dolly Shivani Cherukuri, ameweka rekodi ya kuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi kupata alama 200, katika mashindano yaliyofanyika wiki iliyopita.
288889-2681ba7e-d234-11e4-a4a5-09d7e9cc7466 
Jarida la Press Trust la India, limesema mtoto huyo alirusha mishale 36 kutoka umbali wa mita 5 na mita 7 na kupata alama 388, tukio lililoshuhudiwa na wachezaji wakongwe na maafisa kutoka idara ya kumbukumbu za michezo.
dolly-archer_650x400_81427214935 
Baba yake Cherukuri Satyanarayana ambae ni mmiliki wa club moja inayofundisha kurusha mishale amesema, alimfundisha kurusha mishale tangu alipozaliwa, kwa sasa ana mpango wa kumpeleka kushiriki katika mashindano ili afikie hatua ya kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness.
290181-0a8223fe-d234-11e4-a4a5-09d7e9cc7466
Mcheki kwenye hii video hapa…
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips