
Asubuhi ya leo imeripotiwa stori ya
Askari Polisi wakiwa na silaha kuizunguka nyumba yake, Mbezi Salasala
DAR.. waumini wake, waandishi wa habari pamoja na watu wengine walikuwa
pembeni pia, kuangalia kinachoendelea.
Muda mfupi baadae imeripotiwa kwamba
Askofu huyo alienda Kituo cha Polisi Centre lakini haikuchukua muda
mrefu akatolewa na kupelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu DAR..
kilichokuwa kinaendelea hapo hakuna aliyejua.
Kuna taarifa kwamba Askofu huyo
alitakiwa kuripoti Kituo Cha Polisi jana lakini hakwenda, mashuhuda
wanahisi hiyo ndio sababu iliyofanya Askari kuizunguka nyumba yake leo.
Mvutano uliopo ni kuhusu kuwasilisha
nyaraka za vitu anavyomiliki, lakini amegoma kwenda kuhojiwa mpaka
wapate barua kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment