‘Don’t drink and drive..’ sawa hilo somo jamaa alilielewa sana tuu, akaenda zake kupata kinywaji ishu ikawa jinsi gani atarudi home??
Ilikuwa ni kama bahati yake tu kukutwa
na gari za doria za Polisi ambao walimkuta mida ya saa kumi usiku,
hajielewi.. amelewa sana alafu kalala katikati ya barabara.. hakuwa na
jeraha lolote la kuumizwa wala hakugongwa, kilichomfanya aanguke
katikati ya barabara ni ulevi.
Jamaa aliwaambia Polisi kwamba alitumia usiku wote kulewa, hata hapo alipo hajui kafikaje yani..!!
Ishu metokea New Zealand, ilibidi Polisi
wambebe kumpeleka nyumbani kwake.. Polisi wamesema walevi wengi ni
waathirika wa matukio ya kukabwa na kuibiwa usiku.
Umewahi kukutana na tukio gani mtu wangu na wewe ukasema ulevi noma? Nitafurahi kuona utakachoniandikia kwenye comment yako..
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment