Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Amanda Awa Mbogo Baada ya Kuambiwa Anatumia ARV

Amanda Awa Mbogo Baada ya Kuambiwa Anatumia ARV

Staa mwenye ‘figa’ matata, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni aligeuka mbogo kwa shabiki wake aliyefahamika kwa jina la Joel baada ya kuambiwa eti ni mmoja wa wasanii wanaotumia vidonge vya ARV vya kuongeza siku za kuishi kwa waathirika wa Ukimwi.

Ishu ilianzia kwenye mtandao wa Facebook ambapo Joel aliona picha ya Amanda akipima ugonjwa ambao haukujulikana ndipo kijana huyo alipokomenti kwamba eti msanii huyo ana ngoma.

Akizungumza na mwandishi wetu, Amanda alisema amechoshwa na watu wanaomkashifu mtandaoni wakidhani kila msanii ni mhuni.

“Nimeona nimtolee uvivu kwani asifikirie Bongo Muvi wote tunatumia ARV, mimi nimepima mara ya mwisho juzi na najiamini najua ninachokifanya, alinikera sana yule kijana ndiyo maana nikampa makavu,” alisema Amanda. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips