Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Zitto Kabwe 'Huu ni Mwanzo Mpya Sina Mpango wa Kuendelea Kupigania Uanachama Wangu wa CHADEMA'

Zitto Kabwe 'Huu ni Mwanzo Mpya Sina Mpango wa Kuendelea Kupigania Uanachama Wangu wa CHADEMA'

"Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya hapo juu, ninaomba kukutaarifu wewe na Bunge lako tukufu kwamba sina mpango wa kuendelea kupigania uanachama wangu wa CHADEMA katika viunga vya mahakama.
Kwa hiyo ninatangaza rasmi leo kwamba taratibu za kikatiba zitakapokamilika tu nitaachia uanachama wa CHADEMA, chama nilichokipenda sana kwa sababu ya kuendelea kukua kwa tofauti za kiitikadi, kimtazamo na hata kibinafsi kati yangu na viongozi katika chama changu.
Nimeona kuwa kuendelea kupigania uanachama kisheria ni kutatiza na kukwaza harakati za mabadiliko hapa nchini katika wakati ambapo mfumo wa kisiasa unatambua uwepo wa vyama vingi vya siasa.
Kwa kuwa taratibu hizo sijui zitakamilika lini, natumia fursa hii kuwaaga wabunge wenzangu." WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips