Mchezo
wa mieleka umeonekana kuwa mchezao hatari pengine kuliko michezo yote
licha ya kujizolea umaarufu mkubwa na kupendwa na watu wengi duniani.
Taarifa ikufikikie mtu wangu kuhusu mtoto wa mcheza mieleka maarufu wa Mexico aitaye Hijo del Perro Aguayo ambaye amepoteza maisha wakati alipodondoka jukwani akiwa katikati ya mchezo ikiwa ni saa chache baada ya kukimbizwa hospitali.
Mwanamieleka huyo alikuwa akipigana na mwezake Rey Mysterio
katika pambano lililofanyika ijumaa usiku na mara baada ya kudondoka
alikimbizwa hospitali lakini madaktari walithibitisha kuwa tayari
amefariki.
Wakati akiwa
amedondoka chini wenzake hawakujua kiasi gani ameumia na kuendelea na
mchezo na baada ya dakika zipatazo mbili waligundua kuwa amezidiwa hivyo
kumuwahisha hospitali.
Hapa kuna video ikionyesha wakati pambano hilo linafanyika hadi mwana mieleka huyo alipopoteza fahamu akiwa ulingoni.
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment