Taarifa kutoka nchini Uganda zinasema kuwa mwanamuziki wa Dancehall nchini Uganda anayefahamika kwa jina la AK47amefariki dunia usiku wa leo baada ya kuanguka akiwa bafuni anaoga.
Taarifa zinadai kuwa AK47 amefariki saa 5.30 usiku ya tarehe 16, Machi, 2015 baada ya kukimbizwa katika hospitali ya Nsambya jijini Kampala ambapo taarifa za madaktari zinadai kuwa damu nyingi ilivujia ndani baada ya kuangukia sehemu ya nyuma ya kichwa chake.
AK47 ni kaka wa wanamuziki watatu nchini humo ambao ni Jose Chameleone, Weasel na Pallaso kutoka familia ya Gerald Mayanja na Prossy Musoke.
R. I. P AK47
0 comments:
Post a Comment