Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Taasisi Ya Kiislam Yaitaka Serikali Iwakamate Maaskofu Waliotoa Tamko...Yasema Wasipokamatwa Itahamasisha Waislam Wote Kupiga Kura Ya HAPANA

Taasisi Ya Kiislam Yaitaka Serikali Iwakamate Maaskofu Waliotoa Tamko...Yasema Wasipokamatwa Itahamasisha Waislam Wote Kupiga Kura Ya HAPANA

Taasisi ya dini ya Kiislam imeitaka serikali kuwakamata maaskofu na wachungaji ambao  inadai wametoa matamko ya kichochezi na endapo serikali itashindwa kuwakamata, basi jumuiya hiyo itawahamasisha waamini wa dini ya kiislam popote walipo kuipigia kura yaHapana Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
 
Kauli ya taasisi hiyo yenye misimamo mikali inatokana na Tamko lililotolewa  na muunganiko wa jumuiya ya Kikristo,ikiwemo Baraza la Maaskofu katoliki (TEC),Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT)  na  Baraza la Makanisa la kipentekoste(CPCT) ambao wote  kwa pamoja waliwataka waumini wa dini ya kikristo nchini kuipigia kura ya Hapana katiba inayopendekezwa kutokana na serikali  kuruhusu mahakama ya Kadhi kisheria.
 
Akitoa tamko la Taasisi ya Dini ya Kiislam  ambalo ni muunganiko wa taasisi za dini hiyo zaidi ya 11 hapa nchini,Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh Rajab Katimba wakati wa Mkutano na Vyombo mbalimbali vya habari  jana  Jijini Dar es Salaam, aliitaka serikali kuwachukulia  hatua maaskofu hao kwa madai ya kufanya uchochezi.
 
“Serikali iwachukulie hatua za kisheri maaskofu na wachungaji kwa kutoa matamko yakichochezi yaliyokusudia kuumiza hisia ya kidini kwa waislam kinyume cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.
  
"Tunataka  Maaskofu  hao  wakamatwe,wafikishwe mahakamani na  dhamana  izuiliwe kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali,lasivyo hatutaipigia kura ya Ndiyo katiba iliyopendekezwaalisema Seikh Katimba.
 
Aidha, Sheikh Katimba  aliitaka  Serikali kuendelea na Mchakato wa uundwaji mahakama ya kadhi kwa kufuata maoni yaliyotolewa mbele ya kamati ya sheria na utawala wa bunge kwa kuzingatia mambo muhimu  mawili.
 
Mosi: Serikali iache njama na hila za kuigeuza mahakama ya Kadhi inayohitajika kuwa miliki ya taasisi ya BAKWATA na MUFTI wa BAKWATA.
 
“Endapo serikali itaendelea na kuwasilisha muswaada wa Mahakama ya Kadhi unaoipa mamlaka Bakwata kuunda,kusimamia,kuteua makadhi nakadhalika kinyume na maoni ya Waislam wengi itakuwa imethibitisha kuwa serikali haikuwa na nia ya kweli ya kuunda na kuanzisha mahakama ya Kadhi alisema Sheikh Katimba.
 
Pili: Serikali igharamie mahakama hiyo kama inavyogharimia uendeshaji wa mashauri yaliyopo kwenye mahakama za kawaida yanayohusu sheria za kiislam ambayo mara nyingi yanaamuliwa kwa makosa.
 

Na pia mahakama  hiyo igharamiwe na serikali  kama inavyogaramia huduma za makanisa chini ya mkataba maarufu uitwao memorandum of understanding (MOU) , mkataba  ambao haukuwahusisha wala kutaka ridhaa ya waislam” alisema  sheikh  huyo
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips