Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks
Home » » Ombi Hili la Wema Sepetu, Likufikiae na Wewe….Tubadilike

Ombi Hili la Wema Sepetu, Likufikiae na Wewe….Tubadilike

“Watanzania wenzangu, naombeni leo tujiulize: mitandao ya kijamii ina kazi gani kama sio kuelimisha, kuendeleza na kunufaisha jamii?

Huu ni mwaka 2015. Kama kupendana bure, tushapendana vya kutosha. Kama kutukanana bila sababu, tushatukanana vya kutosha. Kama kushabikia vitu ambavyo havina msaada wowote kwa sisi na familia zetu, tushashabikia vya kutosha.

Imefika hatua ya kunyanyuana, sio kushushana. Kuelimishana, sio kusemana. Kupeana moyo, sio kukatishana tamaa.

Imefika hatua ya kutegemea mabadiliko, na kupigania mabadiliko.

Nakuomba wewe kaka angu, dada angu, mama angu, baba angu...nakuomba ufanye maamuzi leo, kwamba kesho yako haitakua kama jana yako.

Kwa jina naitwa Wema Sepetu. Na leo hii nimeamua kwamba kesho yangu, haitakua kama jana yangu!

Wewe je? “.-Wema  mwenye followers zaidi ya laki nne mtandaoni ameandika haya na kuungwa mkono na mashabiki wengi na hata wale wanomdisi.

Asante sana Wema, ujumbe umefika.

Kwa jina naitwa Mzee wa Ubuyu  na leo hii nimeamua kesho yangu haitakauwa kama jana yangu.

11.03.2015 -  Tags:  WEMA
WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
Weka e-mail yako hapa kupata habari moja kwa moja Karibu sana Usikose kupata habari kwa kutembelea blog yetu Gallos official blog

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Hapa Chini

 
Support : Gallos official blog | Gallos official blog | Gallos official blog
Copyright © 2011. Gallos official blog - All Rights Reserved
Modified by Yuvinusm
Powered by Blogger
Tricks and Tips