Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina kimedai kuwa, Penny na Swedi wanaishi pamoja maeneo ya Mwananyamala jijini Dar na wamekuwa wakioneshana mahaba nilegeze hata mbele za watu huku mara kadhaa wakitupia picha zao za pamoja kwenye mitandao ya kijamii.
“Hivi ninyi mnajua kuwa Penny kapata mrithi wa Diamond? Kama hamjui basi hiyo ndiyo habari ya mjini.
“Kwa taarifa yenu wanapika na kupakua na hakuna asiyejua hilo, kama vipi fuatilieni mtapata ukweli,” alidai mtoa habari huyo.
Katika kujiridhisha, waandishi wetu walianza kufuatilia kwa kufika kwenye nyumba anayoishi Penny na kukuta imefungwa ila baadhi ya majirani walidai kuwa, wanajua uhusiano wa Penny na Swedi kwani wanawaona kila siku wakiingia na kutoka.
Penny alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi ili afunguke juu ya hilo, iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa sms hakujibu hadi tunakwenda mtamboni hivyo jitihada za kumpata ili aweke mambo sawa zinaendelea. WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment