Mabao mawili ya Oliver Giroud katika dakika ya 24 na 28 yalitosha kuipa Arsenal ushindi wa kupiga hatua nyingine mbele.
Kwa upande wa Newcastle bao pekee lilifungwa na Moussa Sissoko kipindi cha pili katika dakika ya 48 ya mchezo.
Ushindi wa Arsenal unakuja ikiwa ni baada ya kutolewa katika klabu Bingwa Ulaya UEFA kwa wastani wa mabao 3-3 dhidi ya Monaco ambapo mchezo wa kwanza walifungwa 3-1 huku mechi ya marudiano walishinda 2-0 na kuifanya Monaco kusonga mbele kwa faida ya goli la ugenini.WEKA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment