‘Nitampata Wapi‘ ni hit ya mkali anayeiwakilisha vizuri TZ kupitia muziki anaoufanya, Diamond Platnumz.. Jina lake sio geni kwa wapenzi wa muziki Afrika.
Ngoma hiyo aliyoitoa mara ya mwisho bado inafanya vizuri.. Wanigeria wanatoa ngoma mpya kila siku, Diamond nae anataka kuwa kama wao?
Kupitia ukurasa wake wa Instagram alishare teaser ya video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Nasema Nawe‘ ambao audio yake tayari iko mtaani halafu akaandika hivi; “Naombeni Ruksa zenu waungwana nianze Kuzifumua…“@diamondplatnumz
Dakika chache baadae ameiweka video hiyo Youtube, kumaanisha kwamba ndio tayari imetoka yani..
Amefanya video nyingi nje ya TZ ikiwemo South Africa na Nigeria.. safari hii VIDEO kaifanya TZ na Director ni Mbongo Hanscana.. Play hapa…
0 comments:
Post a Comment