Mwimbaji wa muziki wa injili, Emmanuel Mbasha, anayekabiliwa na kesi ya kumbaka mtoto wa miaka 17, jana alitoka kwenye chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Ilala akibubujikwa machozi. Hali hiyo ilimtokea mara baada ya shahidi wa pili wa kesi hiyo, aliyejulikana kwa jina la Suzan, kutoa ushahidi wake. Kwa kuwa kesi hiyo inasikilizwa kwenye chemba (chumba maalumu ambacho waandishi na watu wasiohusika hawaruhusiwi kuingia) haikuweza kujulikana mara moja ni kitu gani kilichofanya mwimbaji huyo alie.
Unadhani nini kilichomtoa mchozi jamaa huyu?
0 comments:
Post a Comment